Sinopse
Changu Chako, Chako Changu ni makala inayozungumzia masuala ya historia, utamaduni, muziki na lugha ya Kifaransa Afrika Mashariki na Kati na duniani. Makala haya yatakuhabarisha pia kuhusu Jumuiya ya Kimataifa ya Watu Wanaotumia lugha ya Kifaransa kwenye Mawasiliano (L'OIF) na jinsi gani kujifunza na kuelewa lugha nyingine inaweza kuimarisha mahusiano kwenye sehemu zote za maisha ya binadamu.
Episódios
-
Sehemu ya pili ya makala kuhuus tamasha la watu wa kabila la washi Nov 24 2024
23/11/2024 Duração: 19minMakala haya Ali Bilali anazungumza na msanii Oliver wa nyimbo za asili ya washi wahavu mashariki mwa DRC kuelekea tamasha la Bushi ama Festival de Bushi.
-
Maandalizi ya Tamasha la watu wa Kabila la Washi kutoka Bukavu sehemu ya kwanza.
18/11/2024 Duração: 20min -
Shindano la filamu kwa kutumia simu ya Mkononi na msanii kutoka Mombasa Rojo Mo
09/11/2024 Duração: 19minKaribu katika makala changu chako chako changu Jumapili yaleo ambapo tutakijita zaidi kwenye matokeo ya shindano la kutengeneza filamu kwa kutumia simu ya mkononi liliooandaliwa na Alliance Francaise ya Nairobi nchini Kenya na kwenye Muziki tutakuwa naye msanii kutoka Mombasa Rojo Mo. Mimi ni Ali Bilali Bienvenue ama Karibu, restons ensemble mwanzo hadi tamati, yaani tubaki pamoja mwanzo hadi mwisho.
-
Alliance Francaise ya Nairobi inavyoikuza sanaa ya uigizaji jukwaani sehemu ya kwanza.
04/11/2024 Duração: 19minKatika Makala haya Ali Bilali amejielekeza Alliance Francaise ya Nairobi ambayo imeandaa Onyesho la Kwanza la tamthilia ya ‘Mgonjwa Mwitu’, utayarishaji wao wa kila mwaka wa maigizo yaliyotolewa na tamthilia za waandishi mashuhuri wa Ufaransa. Kwa maadhimisho ya miaka 75, chaguo ni 'Le Malade Imaginaire' na Molière. Hii ni comedy ya mwisho kuandikwa na Molière. Ingawa ilionyeshwa kwa mara ya kwanza mnamo 1673, kichekesho hiki cha kejeli, mojawapo ya bora zaidi za Moliere, hakijapoteza mvuto wake wa dhati na wa ulimwengu wote.Kumbuka pia kumfollow mtangazaji wako @billy_bilali kwenye mitandao ya kijamii @billy_bilali
-
Fahamu hapa kuhusu liliokuwa soko la watumwa nchini DRC Oct 20 2024
04/11/2024 Duração: 20minKaribu katika Makala Changu Chako Chako Changu, ambapo Ali Bilali mtangazaji wako asiependa makuu ameungana na Denise Maheho kutoka Lubumbashi kuzungumzia kuhusu iliokuwa barabara ya watumwa zama za ukoloni.Kumbuka pia kutuachia comment na kumfollow mtangazaji wako asiependa makuu @billy_Bilali kwenye mitandao yake ya kijamii Instagram na facebook.
-
Utamaduni wa ndoa kulingana na kabila la Wameru sehemu ya pili Oct 13 2024
13/10/2024 Duração: 20minAli Bilali ndio jina langu tunakutana tena Jumapili hii katika makala Changu Chako Chako Changu ambapo nakuletea sehemu ya pili ya Makala kuhusu Utamaduni w andoa kulingana na kabila la Wameru, kwenye le parler francophone nitakupa ratiba ya shughuli kwenye vituo vya Alliance Francaise ya Nairobi na Dar es salaam. Na kwenye Muziki tutamaliza na kibao Pambe chake Christian Bella kutoka huko nchini Tanzania, Karibu ama Bienvenue.
-
Utamaduni wa watu wa Kabila la Wameru kutoka nchini Kenya
06/10/2024 Duração: 19minMakala haya mtangazaji wako Ali Bilali anazungumzia kuhusu utamaduni wa watu wa kabila la Wameru kutoka nchini Kenya, wapo pia nchini Tanzania.
-
Utamaduni wa ndoa kabila la wamakonde na wahangaza kutoka nchini Tanzania sehemu ya 2
29/09/2024 Duração: 20minkaribu, Jumapili nyingine kuwa nami katika Makala Changu Chako Chako Changu Makala ambayo hukuletea Historia na utamaduni wa mambo mbalimbali, le Parler francophone na Muziki. Wiki iliopita nilikuletea Utamaduni wa ndoa kutoka makabila ya Wamakonde na wahangaza, ambapo leo nakuletea sehemu ya pili. Na kwenye le parler francophone nitakuletea ratiba za shughuli za kitamaduni kutoka Alliance francaise ya Nairobi na Dar es salaam, Tutamaliza na Wimbo wa Ibrah kutokz Tanzania
-
Utamaduni wa watu wa makabila ya wahangaza na wamakonde kutoka nchini Tanzania
22/09/2024 Duração: 20minKatika makala haya, mtangazaji wako Ali Bilali amezungumza na Amua Rushita kutoka Mkoa wa Mtwara pamoja na Hillary Alexanda Ruhundwa kutoka Mkoa wa Ngara nchini Tanzania kuzungumzia utamaduni wa ndoa kulingana na makabila hayo mawili. Kumbuka pia nawe unaweza kushiriki moja kwa moja studio au kwa njia ya simu. Wasiliana na mtangazaji wako asiependa makuu kufahamu zaidi.
-
Toleo la 11 la Bourse Ghislaine Dupont na Claude Verlon kutolewa huko Benin
26/08/2024 Duração: 19minRFI inaandaa toleo la kumi na moja la Bourse Ghislaine Dupont na Claude Verlon, kwa heshima kwa waandishi wake wawili waliouawa kaskazini mwa Mali Novemba 2, 2013. Bourse hii, ambayo huwafunza waandishi wa habari vijana kumi wa redio na mafundi vijana kumi wa kuripoti kila mwaka, iko wazi. kwa wagombea kutoka nchi zote za Afrika zinazozungumza Kifaransa. Mafunzo hayo yatafanyika Cotonou. Maombi yamefunguliwa hadi Jumapili Agosti 25 saa sita usiku saa za Paris.
-
Changu Chako Chako Changu: Utamaduni wa mahari kwa baadhi ya makabila barani Afrika
26/08/2024 Duração: 19minMakala haya yanaangazia kuhusu gharama ya sherehe za harusi katika karne hii, hususan ukusanyaji wa michango kwa ajili ya kufanaikisha sherehe.
-
Changu chako chako changu Tasnia ya ulimbwende sehemu ya pili
13/08/2024 Duração: 20minKaribu katika makala changu chako chako changu, makala ambayo hukuletea historia ya mambo mbalimbali utamaduni, le parler francophone na Muziki, ambapo leo nakuletea sehemu ya pili ya makala kuhusu Ulimbwende au Model,
-
Changu Chako Chako Changu tasnia ya ulimbwende sehemu ya kwanza Agost 04 2024
04/08/2024 Duração: 20minKaribu katika makala changu chako chako changu, makala ambayo hukuletea mambo mbalimbali ya utamaduni, le parler francophone na Muziki, ambapo leo nakuletea sanaa ya Ulimbwende au Model, na kwenye la parler francophone nitakuletea shughuli zinazoendelea kwenye vituo vya Alliance francaise za ukanda kipindi hiki cha michuano ya Olympiki, mimi ni Ali Bilali Bienvenue.
-
Historia ya kabila la Wabukusu pamoja na sanaa ya muziki kutokea kwa Bendi ya An Noor
21/07/2024 Duração: 20minKaribu kwenye makala ya changu chako ,chako changu juma hili ukiwa nami Florence Kiwuwa. Na kwenye kipengele cha historia hii leo tutaangazia historia ya kabila la Waluhya wanaofahamika kama wabukusu kisha kwenye kipengele chetu cha pili cha LeParle Francophone tutaangazia maonyesho ya Taarab yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Alliance France kisha tutamalizia na mwanamuziki wa Kenya almarufu kama Freshely Mwamburi.
-
Matumizi ya lugha ya kiswahili katika enzi ya Kijiditali
16/07/2024 Duração: 20minKiswahili kinazungumzwa na zaidi ya watu milioni 200 afrika mashariki na kwenye makala haya ya changu chako,chako changu ,Florence Kiwuwa amefanya majadiliano na wanafunzi katika chuo kikuu cha Multmedia ili kujua kuhusu mchango wa lugha hii katika kuendeleza utamaduni na utengamano na vilevile katika kipengele cha muziki amemuangazia mwanamuziki wa Tanzania Harmonize.
-
Changu Chako Chako Changu maalum kuhusu maadhimisho ya miaka 14 ya RFI Kiswahili
07/07/2024 Duração: 19minKaribu katika Makala Changu Chako Chako Changu jumapili ya leo ambapo nakulrtea Makala maalum kuhusu maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 14 tangu Ple RFI Kiswahili ilipoanza kupeperusha matangazo yake mubashara kutoka nchini Tanzania ambapo ilikuwa idhaa ya kwanza ya Kimataifa kutangaza ikiwa Afrika mashariki. Na kwenye Muziki nitakuletea Burudani ya Muziki wa Idd Aziz Kiswahili kitukuzwe wakati huu tukielekea kuadhimisha siku ya Kiswahili duniani. Mimi naitwa Ali Bilali, Bienvenue ama Karibu. Kumbuka pia kumfollow mtangazaji wako Ali Bilali kwa kubonyeza hapa @billy_bilali
-
Changu Chako Chako Changu, maadhimisho ya miaka 64 ya uhuru wa DRC
06/07/2024 Duração: 20minMakala haya Ali Bilali anazungumzia kuhsu maadhimisho ya miaka 64 ya Uhuru wa DRC.
-
CHANGU CHAKO CHAKO CHANGU HISTORIA NA UTAMADUNI WA WATU WA KABILA LA WANUBI
16/06/2024 Duração: 20minEid Mubaraka kwako mskilizaji wa RFI Kiswahili popopte pale ulipo ausubuhi hii. Karibu kuungana nami katika Makala haya Changu Chako Chako Changu. Leo nakuletea Historia ya watu wa Kabila la Wanubi, na kwenye Muziki nakupeleka nchini Burundi ambapo nazungumza na msanii wa kizazi kipya, Keypeacvaldiny. mimi ni Ali Bilali mtangazaji wako asiependa makuu Karibu ama bienvenue. Jina lake halisi ni Nzeyimana touré hamissi, anatumia jina la kisanii a @keypeac_valdyn amezaliwa April 8 mwaka 2002 jijini Bujumbura inchini burundiAlianza muziki mwaka 2017, ila sababu ya harakati za masomo na familia alilazimika kuachana kabisa na muziki na kujikita zaidi na masomo. Baada ya kumaliza shule mwaka 2023 akaamuwa kurejea kwenye tasnia ya Muziki ambapo amekuja na EP yake iliowekwa hewani tangu April 15 mwaka 2024. EP yake hiyo ina nyimbo 3 ambazo ni:Track n°1.carolinaTrack n°2.sorryTrack n°3.mmmhna songs hizo zote zipo kwenye platforms zake zote anapatikana kwa jina la @keypeac valdynyupo kwenye platforms zifwatazo kama : a
-
Historia ya madaraka Day nchini Kenya na ziara ya Mistachampagne studio za RFI Kiswahili
04/06/2024 Duração: 20minKaribu katika makala ya leo changu chako chako changu ambapo leo nakuletea historia ya siku ya madaraka ambayo huadhimishwa kila Juni Mosi nchini Kenya. Na kwenye le parler francophone kama kawaida nakuletea ratiba ya shughuli za kitamaduni Alliance francaise za ukanda. Na Kwenye Muziki nitakuwa naye Mr Champagne msanii kutoka nchini Burundi ambaye yupo nchini Kenya kwa ajili ya kutangaza wimbo wake mpya Niko tu. Mimi ni Ali Bilali bienvenue ama karibu. Kumbuka pia kumfollow mtangazaji wako kwenye mitandao ya kijamii @billy_bilali
-
Historia na utamaduni wa kabila la wanyakyusa sehemu ya pili
30/05/2024 Duração: 20minKaribu katika Makala haya changu chako chako changu, jumapili ya leo ambapo nakuletea awamu ya pili ya makala kuhusu historia na utamaduni wa watu wa kabila la Wanyakyusa, na kwenye Muziki nakupa muendelezo wa mazungumzo na wasanii Kidum Kibidon na EstherNish. Mimi ni Ali Bilali. Bienvenue.