Siha Njema

Changamoto za afya ya akili miongoni mwa watoto na vijana Afrika

Informações:

Sinopse

Kumekuwa na ongezeko la idadi ya watoto na vijana wanaokabiliwa na changamoto za  afya  ya akili Kila mwezi Mei dunia huungana kufanya kampeni ya watu kuwa makini na afya zao za akili ili kuzuia changamoto zaidi za akili ambazo wakati mwingi huishia kwenye umauti na matatizo zaidi ya kiafyaWatalaam wa afya wanasema watoto na vijana pia nao hupatwa na changamoto hizi zinazohusishwa na afya ya akili ,matatizo hayo yakiwemo kiwewe na msongo wa mawazo.Daktari bingwa wa afya ya akili katika hospitali ya rufaa ya Kenyatta kitengo cha watoto ,Dkt Josephine Omondi anasema mazingira yanayochochea hali hii ni mizozo ya kifamilia ,matumizi mabaya ya mitandao ,shinikizo kutoka mazingira ya shule na pia matatizo ya kiafya yanayohusishwa na miaka ya awali ya mtotoMshauri Nasaha Naomi Ngugi anasema ni wakati wazazi wakakumbatia ukweli kuwa watoto na vijana huhitaji washauri nasaha na matibabu mengine ya matatizo ya afya ya akili