Sinopse
Katika mfululizo wa vipindi vyetu utapata fursa ya kujifunza kuhusu masuala ya uchumi na biashara pamoja na mazingira.
Episódios
-
Mti unapoanguka… - Kukatwa kwa misitu barani Afrika
13/03/2014 Duração: 12minAfrika ina kiwango kikubwa cha ukataji misitu kuliko mabara mengine yote duniani. Hili lina athari kubwa kwa maisha ya Waafrika kama hawa katika mchezo wetu wanaoishi katika kambi ya wakimbizi baada ya vita vya kikatili.
-
Anasa ya Kuazima – Hatari ya Kuchukua Mkopo
06/08/2013 Duração: 11minTatizo linaanzia na ari ya kutaka kumiliki baiskeli mpya ya kifahari. JD hana fedha za kutosha lakini anashindwa kuvumilia na kuchukua mkopo – ingawa hajui atakavyoulipa mkopo huo. Je, somo hili litamuathiri vipi JD?
-
Ufisadi - Tembo chumbani
06/08/2013 Duração: 11minIwe shuleni, kazini au hata barabarani, familia ya Odhiambo inajikuta ikishinikizwa na athari za ufisadi licha ya juhudi za kutaka kuishi maisha huru yasiyo na dosari ya uovu huu. Watawezaje kuepukana na vitendo hivyo?
-
Wajasirimali wa kiafrika – Wenye mafanikio na wenye kuwajibika
10/05/2012 Duração: 11minHulala kidogo sana, hawafahamu neno „starehe“ lakini wanaipenda kazi yao na wanajitoa kwa jamii wanamoishi. Hili ni jambo linalowaunganisha wafanyabiashara wote wa Kiafrika tunaowatambulisha katika mfululizo wetu mpya.
-
Utandawazi - Rafiki na adui wa Afrika
25/05/2011 Duração: 09minVipindi vya Noa Bongo vinachunguza kwa kina athari za utandawazi barani Afrika. Kupitia vipindi vyetu wasikilizaji wanaweza kukutana na watu wanaochangia kuufanikisha utandawazi na wale wanaoathiriwa na utandawazi.
-
Uhamiaji mijini – Kipindi 10 – Habari nzuri sana
16/03/2011 Duração: 11minKatika awamu ya mwisho ya safari, tunaona mabadiliko katika hadithi wakati Tingo anapoonyesha nia ya dhati katika chama. Baki na Zeina wanapatana kwa kinywaji. Tujiunge nao!
-
Uhamiaji mijini – Kipindi 09 – Fikra zilizogubikwa na wingu jeusi
16/03/2011 Duração: 12minTingo hafurahii ufanisi wa chama na huenda akawa na njama fulani. Hii itakuwa na maana gani kwa mashujaa wetu?
-
Uhamiaji mijini – Kipindi 08 – Furaha ya mapenzi
16/03/2011 Duração: 12minHadari amebadili nia na Baki amebadili mipango – hatua inayomfurahisha sana Zeina. Tufuatilie mabadiliko yote yanayoendelea.
-
Uhamiaji mijini – Kipindi 07 – Kushindwa kwa rushwa
16/03/2011 Duração: 12minKatika kipindi hiki Baki anapelekwa hospitalini – nini kilichotokea? Lakini kwanza tutafute jinsi chama kinavyoendelea na vipi mashujaa wetu chipukizi wanavyokabiliana na changamoto.
-
Uhamiaji mijini – Kipindi 06 – Kukabiliwa na vikwazo huku ukiniwa na shinikizo
16/03/2011 Duração: 12minKwa nini Ben anakataa pendekezo zuri kutoka kwa Tingo, ingawa chama kinahitaji fedha? Kipindi kinapofikia tamati, kitu kingine kinaendelea kati ya Ben na Nana.
-
Uhamiaji mijini – Kipindi 05 – Umuhimu gani wa kuwa sahihi iwapo uko peke yako
16/03/2011 Duração: 12minMpaka sasa kila kitu kinaonekana kwenda kulingana na mpango. Wanakijiji wanauonaje mradi huo? Tunaungana na mashujaa watatu katika mkutano na Hadari na tusikilize huku wakifanya mkutano wao wa kwanza wa mwaka.
-
Uhamiaji mijini – Kipindi 04 – Ndoto ya kila mwanamke
16/03/2011 Duração: 12minHatua kwa hatua, marafiki zetu wanapiga hatua wanapojaribu na kuungwa mkono na wanakijiji. Hata hivyo uhusiano kati ya Baki na Zeina unaonekana ukichukua mkondo tofauti.
-
Uhamiaji mijini – Kipindi 02 – Kuwa na majukumu uhamishoni
16/03/2011 Duração: 12minUngana na marafiki zetu wanapofikiria kuvumbua mpango wa biashara kwa chama chao cha kilimo. Lakini Baki ana jambo lengine akilini mwake.
-
Uhamiaji mijini – Kipindi 03 – Kipato cha kila siku
16/03/2011 Duração: 12minBaki, Zeina na Ben wanataka kuanza kwa ufanisi. Kwa bahati mbaya kurejea kijijini huenda kusiwe rahisi kama inavyoonekana na si kila mtu anafurahia kuwaona.
-
Uhamiaji mijini– Kipindi 01 –Bila kazi mjini hakufai
16/03/2011 Duração: 12minKatika vipindi hivi vipya, Ben, Baki na Zeina watatueleza matukio yasiyo ya kawaida wanapoamua kuondoka mjini kwenda kijijini kutimiza ndoto zao.
-
Mazingira Afrika – Kipindi 10 – Vyakula vya baharini
16/03/2011 Duração: 09minKwa nini ni muhimu kuwafundisha wavuvi kutumia nyavu ili kuwalinda kaa? Juhudi gani zinaweza kuchukuliwa kuwalinda Papa? Sikiliza na ufahamu zaidi juu ya hilo na mengine.
-
Mazingira Afrika – Kipindi 9 – Uvuvi wenye madhara
16/03/2011 Duração: 09minKipindi hiki kinazungumzia uvuvi wa kutumia baruti unavyoathiri matumbawe ambayo yanahitaji karne kujengeka, lakini yanaweza kuharibiwa kwa sekunde moja tu. Nini kinachowakumba wanyama na mimea ya baharini?